Watu 961 wakutwa na corona, 854 wapona

0

Watu 961 wamepatikana virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya kupima sampuli 7,780 na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 85,130.

Mtoto wa miezi mitano pamoja na ajuza mwenye umri wa miaka tisini na nne ni miongoni mwa wale waliopatikana na ugonjwa huo.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema wagonjwa wengine 854 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona 56,464.

Wagonjwa 10 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya maafa nchini 1,484.

Nairobi imeandikisha visa 203, Nakuru 118, Kilifi 83, Kirinyaga 71, Kericho 57 Uasin Gishu 52.

Jijini Nairobi, Lang’ata imeandikisha visa (26), Kibra (24), Mathare (19), Dagoreti North (17), Makadara (14) na Kasarani (13).

Aidha wagonjwa 1,240 wamelazwa katika hospitalini tofauti, wanaoshughulikiwa nyumbani ni 7,755.

Wagonjwa waliolazwa katika chumba cha watu mahututi ni 74 huku 40 wakisaidiwa na mashine kupumua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here