Watu 810 wakutwa na corona

0

Watu 810 wamepatikana na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya sampuli 7,387 kupimwa na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 79,322.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema wagonjwa 49 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi 14 wakisaidiwa na mashine kupumua.

Watu wengine 265 wampeona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 52,974.

Idadi ya maafa nchini imeongezeka na kufika 1,417 baada ya wagonjwa 8 zaidi kufariki.

Msambao wa visa hivyo nikama ifuatavyo Narobi 252, Mombasa 77, nakuru 38, Uasin Gishu 36, Siaya 34, Nyandarua 31, Kericho na Busia 30 na Nyamira 29.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here