Watu 7 wafariki katika ajali Kaburengu

0

Watu 7 wamefariki na wengine 14 kujeruhiwa baada ya lori kupoteza mwelekeo na kuwagonga wafanyibiashara katika eneo la Kaburengu kwenye barabara kuu ya Eldoret-Webuye.

Akidhibitisha ajali hiyo, kamanda wa Polisi Kakamega James Ngetich amesema lori hilo lililokuwa linaelekea Webuye lililopoteza mwelekeo na kuwagonga wachuuzi hao waliokuwa wanaouza bidhaa zao kando kando mwa barabara.

Uchunguzi umeanzishwa kubaini ni vipi dereva wa lori hilo alishindwa kulidhibiti na kusababisha ajali hiyo.

Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Webuye kwa matibabu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here