Idadi ya waliopona ugonjwa wa corona hapa nchini imeongezeka na kufikia 32,084 baada ya watu wengine 227 kupona ugonjwa huo katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Kati ya watu hao, 146 walikuwa nyumbani huku wengine 81 wakiruhusiwa kuondoka katika hospitali mbalimbali amesema waziri wa afya Mutahi Kagwe.
Waziri Kagwe amesema idadi ya maafa imeongezeka na kufikia 839 baada ya watu 7 zaidi kufariki.
Aidha, mtoto wa miezi mitano ni miongoni mwa watu 195 waliokutwa na ugonjwa huo katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya kupima sampuli 1,852 na kufikisha idadi ya visa hivyo nchini kuwa 45,076.
Wagonjwa wa corona walio katika vyumba vya watu mahututi ICU ni 39, waliolazwa katika hospitali mbali nchini ni 1,084 huku wanaoshughulikiwa nyumbani wakiwa 2,480.
Nairobi inaongoza katika msambao kwa kuwa na visa 99, Busia 18, Uasin Gishu 17, Meru 14, Mombasa & Kiambu 10, Murang’a 8, Nakuru 7, Kajiado 3, Kisumu & Machakos 2, Bungoma, Wajir, Kitui, Nyandarua & Nandi 1.