Aliyekuwa mbunge wa Makadara Benson Mutura na aliyekuwa spika wa bunge la Nairobi Alex Ole Magelo ni miongoni mwa watu 7 walioorodheshwa kuwania nafasi ya spika wa bunge hilo kufuatia kujiuzulu kwa Beatrice Elachi.
Wengine ni pamoja na; Abdi Ali, Odingo Washington, Mike Guoro, Allan Mang’era pamoja Kennedy Ng’ondi.
Wawakilishi wadi wa bunge hilo wanatazamiwa kukutana hapo kesho Ijumaa kumchagua spika wao.
MCA wa Ruai John Kamangu anashikiliza wadhifa huo kwa muda kufuatia kujiuzulu kwa Elachi aliyedai kuhofia maisha yake.