Watu 671 wamepatikana na corona

0

Watu 671 wamepatikana na corona baada ya kupima sampuli 6,200 katika  muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema hii inafikisha 23,873 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini.

Aidha, watu 603 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 9,930 huku watu 3 zaidi wakifariki na kufikisha idadi ya maafa kuwa 391.

Waziri Kagwe kwa mara nyingine amewarai Wakenya kuwa makini ili kuepuka msambao wa ugonjwa huo huku akitoa mfano wa familia moja huko Migori ambapo watu 48 wamepatikana na ugonjwa huo.

Katika msambao wa visa hivyo, Nairobi ingali kifua mbele kwa kurekodi visa 376, Kiambu 112, Machakos 20, Kisumu 15 na Mombasa 6.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here