Watu 650 wapatikana na corona, Nairobi ikiendelea kuongoza

0

Wakenya 633 na raia 17 wa kigeni ni miongoni mwa watu 650 waliopatikana na ugonjwa wa corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Katibu katika wizara ya afya Mercy Mwangangi anasema watu hao wakiwemo wanaume 391 na wanawake 259 wamepatikana na ugonjwa huo baada ya kupima sampuli 6,768 na hivyo kufikisha idadi ya visa hivyo nchini kuwa 28,754.

Watu wengine 490 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 15,100 huku maafa yakifikia 460 baada ya wagonjwa 4 zaidi kufariki.

Nairobi imeandikisha 356, Kiambu 53, Nakuru 48, Machakos 26, Kajiado & Busia 20, Uasin Gishu & Laikipia 15, Bomet 10, Bungoma 9, Migori, Mombasa & Kisii 7, Tharaka Nithi 6, Murang’a, Narok & Turkana 5, Kericho, Makueni, Kitui & Samburu 4.

Kufikia sasa, Nairobi inaongoza kwa kuwa na visa 16,781, Mombasa ni ya pili kwa visa 2,189, Kiambu 2,078, Kajiado 1,575, Machakos 1,015, Busia 865, Nakuru 604 na Uasin Gishu 348.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here