Watu 570 wapona corona Kenya

0

Kenya imerekodi idadi kubwa  ya wagonjwa waliopona virusi vya corona baada ya watu 570 kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema hii inafikisha 3,638 idadi ya watu waliopona huku visa vipya 421 vikiripotiwa na kufikisha idadi hiyo kuwa 11,673.

Hata hivyo idadi ya maafa imeongezeka na kufikia 217 baada ya wagonjwa wanane kufariki katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Kaunti 42 kati ya zote 47 zimerokodi visa vya ugonjwa huo huku Nairobi ikiongoza kwa kuwa visa 6, 491, Mombasa ni ya pili kwa kuwa na visa 1,783, Kiambu ni ya tatu kwa kuwa na visa 640.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here