Watu 561 zaidi wameambukizwa virusi vya covid 19

0

Watu 561 zaidi wameambukizwa virusi vya covid 19 baada ya kupima sampuli  6,387 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maambukizi kuwa 89,661.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amedhibitisha kupona kwa watu wengine 355 na kufikisha idadi hiyo 70,194.

Aidha wagonjwa wengine 7 wamefariki na kufikisha idadi ya watu walioaga kuwa 1,552.

Wagonjwa 1,096 wamelazwa katika hospitali mbalimbali, 8,016 wanahudumiwa nyumbani, 63 kwenye chumba cha watu mahututi ICU huku wengine 43 wakisaidiwa na mashine kupumua.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifuatavyo; Nairobi 189, Mombasa 85, Bungoma 65, Busia 36, Kericho, Kiambu, Kwale 19 na Kisumu 17.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here