Watu 426 wapatikana na corona

0

Idadi ya visa vya ugonjwa wa corona nchini imeongezeka na kufikia 31,441 baada ya watu 426 kupatikana na ugonjwa huo katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Watu hao wanajumuisha raia tisa wa kigeni wamepatikana na ugonjwa huo baada ya kupima sampuli 5,158 anavyoeleza katibu katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi.

Watu wengine 257 wameruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 17,869 huku maafa yakifikia 516 baada ya kufariki kwa watu 10 zaidi akiwemo mtoto wa miaka mitatu.

Nairobi inaongoza katika msambao wa visa hivyo kwa kurekodi visa 132, Kajiado 63, Kericho 48, Kilifi 24, Machakos 21, Migori 17, Laikipia & Kitui 13, Nakuru & Kisumu 11.

Langata inaongoza Nairobi kwa kuripoti visa 22, Westlands 14, Embakasi East 12, Kibra 11, Dagoreti North & Makadara 8, Embakasi West, Kasarani & Starehe 7.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here