Watu 413 wakutwa na corona, 12 wafariki

0

Watu 413 wamekutwa na corona baada ya kupima sampuli 3,489 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Hii inafikisha 77,785 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kufikia sasa.

Nairobi imerekodi visa 229, Mombasa 46, Kiambu 22, Busia 18, Uasin Gishu 15.

Waliopona katika muda huo ni 396 na hivyo kufikisha idadi hiyo kuwa 51,903.

Idadi ya maafa yanayotokana na ugonjwa huo imefikia 1,392 baada ya kufariki kwa wagonjwa 12 zaidi.

1,182 ndiyo idadi ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali huku 7,142 wakishughulikiwa nyumbani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here