Watu 373 wapatikana na corona

0

Watu 373 zaidi wamepatikana na virusi vya corona baada ya kupima sampuli 4,663 na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 33,389.

Katibu mkuu wa wizara ya afya Dkt. Rashid Aman amesema kuwa visa vya maafa vimeongezeka na kufikia 572 baada ya watu 3 zaidi kuaga.

Dkt. Aman amesema kuwa watu 72 wamepona kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona nchini kuwa 19,368.

Kaunti Nairobi inaongoza kwa kurekodi visa 117, Busia 66, Nakuru 37, Kisii 32, Homabay 15, Kiambu 12, Kisumu 11, Uasin Gishu 8, Garissa, Narok, Taita Taveta na Isiolo 7, Mombasa 6, Murang’a na Migori 5, Kirinyaga  4 , Nyeri, Nandi, Machakos na Kericho 3, Bomet, Kakamega na Kitui 2, Meru, Makueni, Siaya, Turkana na Nyamira 1.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here