Madaktari wanane ni miongoni watu 274 waliofariki kutokana na ugonjwa corona mwezi huu pekee amesema waziri wa afya Mutahi Kagwe.
Kagwe ambaye amesema wahudumu wa afya watapewa bima vile vile ametangaza kuwa watu 18 zaidi wamefariki katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maafa kuwa 1,287.
Aidha, taifa limeandikisha visa vipya 559 vya ugonjwa huo baada ya kupima sampuli 3,074 na kufikisha idadi hiyo kuwa 70,804.
Idadi ya waliopona imefikia 46,244 baada ya kupona kwa watu wengine 478.