Kenya imerokedi visa vipya 213 vya ugonjwa wa corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya visa hivyo nchini kuwa 33,016.
Rais Uhuru Kenyatta katika hotuba yake kwa taifa aidha ametangaza kwamba idadi ya waliopona ugonjwa huo imefikia 19,296 baada ya kupona kwa watu 241.
Maafa yanayotokana na ugonjwa huo wa COVID19 imeongezeka na kufikia 564 baada ya kufariki kwa wagonjwa watano zaidi katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi 101, Mombasa 19, Busia 17, Kiambu 12, Machakos 8, Kajiado 7, Isiolo 5, Kericho 6, Meru 5, Bomet 4, Samburu, Bungoma, Kilifi, Kirinyaga, Kisii 3, Kisumu, Murang’a, Lamu, Nakuru & Makueni 2.