Watu 19 zaidi wafariki kutokana na corona

0

Maafa yanayotokana na ugonjwa wa corona yamezidi 500 baada ya wagonjwa 19 zaidi kufariki katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Katibu katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi anasema idadi hiyo imefikia mia tano na sita huku wengi wa waliofariki wakiwa wanaugua magonjwa mengine kama vile kisukari na shinikizo la damu.

Aidha idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini imefikia 31,015 baada ya visa vipya 379 kuripotiwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita huku waliopona wakifikia 17,612 baada ya kupona kwa watu wengine 244.

Nairobi 219, Kiambu 40, Uasin Gishu 28, Kajiado 14, Machakos 13, Kisumu 10, Mombasa 7, Kericho 6, Baringo & Bomet 5, Nandi & Nyeri 4, Isiolo & Narok 3, Busia, Garissa, Homabay & Kilif 2.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here