Idadi ya visa vya ugonjwa wa corona nchini imeongezeka na kufikia 28,104 baada ya watu 679 kukutwa na ugonjwa huo katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya kupima sampuli 6,590.
Miongoni mwa watu hao ni mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na mzee mwenye umri wa miaka 87 kwa mujibu wa katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi.
Watu wengine 743 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 14,610 huku maafa yakiongezeka na kufikia 456 baada ya wagonjwa 18 zaidi kufariki akiwemo meneja wa KEMRI Kamau Mugenda.
Nairobi imerekodi visa 349, Kiambu 69, Kajiado 35, Machakos 25, Nyeri 23, Garissa 18, Mombasa 16, Kericho 14, Uasin Gishu & Nyandarua 13, Tharaka Nithi 11, Laikipia 9, Nakuru & Migori 8, Kisumu 7, Nandi & Busia 6, Meru 5, Muranga, Kirinyaga, Makueni & Isiolo 4.