Watu 16 zaidi wafariki kutokana na corona

0

Watu 16 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa wa corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 858.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe katika taarifa amesema visa vipya 497 vimedhibitishwa baada ya kupima sampuli 4,888 na kufikisha idadi hiyo kuwa 46,144.

Nairobi imeandikisha visa 227, Machakos 64, Mombasa 51, Uasin Gishu 37, Laikipia 28 na Busia 19.

Watu wengine 238 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 32,760.

Wagonjwa walio katika chumba cha watu mahututi ni 27, wanaosaidiwa na mashine kupumua ni 41.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here