Watu 16 wafariki kutokana na corona

0

Kenya kwa mara ya kwanza imeandikisha idadi kubwa ya maafa yanayotokana na ugonjwa wa corona baada ya kufariki kwa watu 16 kwa siku moja.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema hii inafikisha 341 idadi ya maafa ya yanayotokana na ugonjwa huo kufikia sasa.

Na huku idadi ya maafa ikiendelea kupanda, waziri Kagwe amewatahadharisha Wakenya dhidi ya kudhania kuwa wanaokufa ni wazee pekee au watu waliokuwa na magonjwa mengine.

Aidha, idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini imefikia 20,636 baada ya watu 723 kupatikana na ugonjwa huo huku waliopona wakifikia 8,165.

Nairobi 436, Nakuru 83, Mombasa 48, Kiambu 45, Turkana 12, Uasin Gishu 10, Machakos & Kajiado 9, Busia 8, Muranga & Kericho 7, Kisumu 6, Baringo & Bomet 5, Garissa, Kwale, Nyeri & Siaya 3, Isiolo, Kakamega, Lamu, Meru, Wajir, Taveta, T. River, Vihiga & 2, Nyandarua, E. Marakwet, Makueni, Marsabit, & Kilifi 1.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here