Watu 151 zaidi wakutwa na corona, nne wakifariki

0

Idadi ya visa vya ugonjwa wa corona nchini imeongezeka na kufikia 38,529 baada ya watu 151 kupatikana na ugonjwa huo kufuatia kupimwa kwa sampuli 2,927 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Katibu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman amesema idadi ya waliofariki imeongezeka na kufikia 711 baada ya kufariki kwa watu wanne zaidi huku waliopona wakifikia 24,908 baada ya kupona kwa watu 168.

 Nairobi imeandikisha visa 32 kati ya visa hivyo, Kisumu 22, Garissa 14, Mombasa 10, Meru & Kajiado 8, Kisii 6, Bomet & Kiambu 5,  Siaya 3, Uasin Gishu, Kilifi, West Pokot, Murang’a, Marsabit 2, Kakamega, Bungoma, Kitui & Nyamira 1 kila mmoja.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here