Watu 148 wameambukizwa virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya sampuli 2,438 kupimwa na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 36,724.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe katika taarifa amedhibitisha kuwa watu 98 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona nchini kuwa 23,709.
Wakati uo huo idadi ya maafa yanayotokana na ugonjwa huo imeongezeka na kufika 646 baada ya watu wengine wanne zaidi kufariki.
Mombasa inaongoza kwa kuandikisha visa 40 vya ugonjwa huo, Nairobi 32, Laikipia 15, Kiambu 11, Nakuru na Embu 7, Uasin Gishu na Kajiado 6, Taita Taveta na Kisumu 5, Kitui 4, Trans Nzoia 3, Baringo, Elgeiyo Marakwet, Kwale, Machakos, Kericho, Makueni na Murang’a kisa kimoja kila mmoja.