Watu 1,470 zaidi wakutwa na corona Kenya

0

Watu 1,470 zaidi wamedhibitishwa kuambukizwa virusi vya covid 19 baada ya sampuli 8,072 kupimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita hivyo kufikisha idadi ya  ya maambukizi kuwa 68,193.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amedhibitisha kupona kwa wagonjwa 791 zaidi na kufikisha idadi ya waliopoa kuwa 44,872. Wagonjwa 695 walikuwa wakihudumiwa nyumbani na 96 walikuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali.

Wagonjwa 25 zaidi wamefariki kutokana na makali ya ugonjwa huo na kufikisha idadi ya maafa kuwa 1,228.

Kufikia sasa watu 1,364 wamelazwa katika hospitali mbalimbali na 5,726  wanahudumiwa nyumbani.

Walio katika vyumba vya wagonjwa mahututi ICU ni 54 na 32 wanasaidiwa na mashine kupumua.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifuatavyo; Nairobi inaongoza na 649, Mombasa 183, Kilifi 124, Kiambu 77, Kericho 75, Kakamega 37, Kajiado 31, Busia 30, Uasin Gishu 24, Machakos 24, Kisii 22 na Nakuru 19.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here