Watu 141 wapatikana na corona

0

Kwa mara ya kwanza kaunti ya Trans Nzoia imeandikisha idadi kubwa ya virusi vya corona huku visa 141 vikiripotiwa baada ya kupima sampuli 3,307 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Katibu katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi anasema hii inafikisha 37,489 idadi ya visa vya ugonjwa huo kufikia sasa.

Watu wengine 81 wamepona kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 24,334 huku maafa yakifikia 669 baada ya kufariki kwa watu watano zaidi.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Trans Nzoia 28, Nakuru 24, Nairobi 14, Mombasa 14, Kiambu 9, Migori 8, Kisumu & Kajiado 6.

Wakati uo huo

Kaimu mkurugenzi wa huduma za matibabu Dkt. Patrick Amoth amesema kuzingatiwa kwa masharti ya usalama kuzuia msambao wa virusi hivyo vya corona ikiwemo kunawa mikono na kuvalia barakoa kumesaidia kuokoa maisha ya watu zaidi ya alfu nne ambao wangefariki kufikia mwishoni mwa mwaka huu kutokana na virusi hivyo.

Aidha, wahudumu wa afya wapatao 954 wameambukizwa virusi hivyo kufikia sasa huku 16 kati yao wakifariki.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here