Watu 14 zaidi wafa kutokana na corona, watu 836 wakiambukizwa

0

Idadi ya wagonjwa wanaofariki kutoka na ugonjwa wa corona inaendelea kuongezeka huku wagonjwa 14 zaidi wakipoteza maisha katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema idadi hiyo sasa imefikia 934 huku 38 wakiwa katika chumba cha watu mahututi.

Na baada ya kupima sampuli 4,076, watu wengine 836 akiwemo mtoto wa miezi minne wamekutwa na virusi hivyo na kufikisha idadi ya visa hivyo nchini kuwa 50,833.

Nairobi imeandikisha visa 556, Lang’ata 295 na Kibra 43, Uasin Gishu 68, Mombasa 62, Kiambu 32 na Nakuru 24.

Waliopona wamefikia 34,832 baada ya watu 403 kupona, 250 wakipona wakiwa nyumbani na wengine 153 wakiruhusiwa kuondoka katika hospitali mbalimbali.

Wagonjwa waliolazwa hospitalini kote nchini ni 1,150, huku wengine 3,961 wakishughulikiwa wakiwa nyumbani.

Hayo yakijiri

Chama cha Matatibu nchini (KUCO) sasa kinasema wanachama wake wapatao 300 wameambukizwa virusi vya corona.

Kupitia mwenyekiti wake Peter Wachira, matibabu hao wamesema kulegezwa kwa masharti ya kuzuia msambao wa virusi hivyo kumeishia kuhatarisha maisha ya wahudumu hao wa afya.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here