Watu 13 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa wa corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 682 kufikia sasa.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe katika taarifa amedhibitisha kuwa watu wengine 218 wameambukizwa virusi hivyo baada ya kupima sampuli 5, 424 na kufikisha idadi ya maambukizi kuwa 37,707.
Aidha watu 170 wamedhibitishwa kupona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 24,504.
Msambao wa visa hivyo ni kama ifuatavyo: Nairobi inaongoza kwa kurekodi visa 68, Kisii 28, Mombasa 21, Kisumu 19, Kajiado 11, Busia 10, Machakos 8, Tharaka Nthi, Garissa 6, Laikipia, Kakamega na Kericho 2, Murang’a, Bomet na Kilifi wamerekodi kisa kimoja.