Raia wa Tanzania wanaowasili nchini hawatalazimika kujitenga kwa muda wa siku kumi na nne.
Hii ni baada ya mamlaka ya safari za angani KCAA kutoa orodha mpya ya mataifa 147 ambayo raia wake wanaowasili nchini hawatajitenga kwa muda wa siku kumi na nne kabla ya kutangamana na raia wengine.
Hatua ya Kenya kuwalazimu watanzania wanaowasili nchini kujitenga ilionekana kuibua mzozo wa kidiplomasi baina ya mataifa hayo mawili na kusababaisha Tanzania kupiga marufuku ndege za Kenya kwenye anga zake.
Mataifa haya mawili yamekosa kuelewana kuhusiana na masharti ya kupambana na virusi vya corona huku Rais John Pombe Magufuli akitangaza kuwa Tanzania haina tena virusi vya corona.