Washukiwa wawili wakamatwa kwa ukora

0

Washukiwa wawili wamekamatwa kwa kupanga njama ya kumuibia mbunge wa Kasipul Charles Ong’ondo Were wakijifanya kuwa makachero wa idara ya upelelezi DCI.

Wawili hao Dennis Muturi Nyakundi na Victor Onsare walikuwa wamemtaka mbunge huyo kufika katika makao makuu ya DCI kuhojiwa.

Hata hivyo Nyakundi na Onsare baadaye walimpigia simu mheshimiwa huyo wakihairisha mahojiano hayo ila wakamtaka kukutana nao katika hoteli moja kwa mazungumzo.

Mbunge huyo alishuku nia yao aliripoti tukio kwa Polisi ambao hatimaye waliwawekea mtego na kuwashika.

Wawili hao sasa watafikishwa mahakamani kushtakiwa kwa kujaribu kumuibia mbunge huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here