Washukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevywa washikwa

0

Makachero wa idara ya upelelezi DCI wamewashika washukiwa wawili walanguzi wa dawa za kulevya.

Washukiwa hao wamenaswa wakisafirisha bangi yenye dhamana ya mamilioni ya pesa kuelekea Nairobi kutoka Namanga.

Wawili hao Samwel Kimani na Peter Mwangi watafikishwa mahakamani kesho kushtakiwa.

Kwingineko

Washukiwa watatu waliokuwa wamemteka nyara mwanamke mmoja wamekamatwa na makachero wa DCI katika kaunti ya Narok.

Watatu hao Rose Waithera, Jackson Kamau na Julius Guchu wameshikwa katika eneo la Siyapei ambapo walikuwa wamejificha kwenye msitu.

Mali waliyokuwa wamemuibia mwathiriwa ikiwemo pesa alizokuwa ametoa kwa benki imepatikana.

Washukiwa hao wanazuiliwa wakisubiri kufikishwa mahakamani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here