Washukiwa wa uhalifu wanaswa Bungoma

0

Washukiwa wawili wa uhalifu wanatazamiwa kufikishwa mahakamani hii leo kukabiliwa na tuhuma za wizi wa mabavu.

Washukiwa hao, Martin Simiyu Wabale na Richard Wekesa Wafula, wanadaiwa kumwibia mwanaume mmoja mtaani Karen, Nairobi kabla ya kutorokea mafichoni eneo la Kimilili, kaunti ya Bungoma, ambapo walitiwa mbaroni.

Idara ya upelelezi nchini DCI inasema washukiwa hao wamekuwa wakiwahadaa watu kuwa wangewapatia kazi na badala yake kuwapelaka eneo halina watu na kuwapora mali yao.

Kwa mfano mwezi Agosti mwaka huu, washukiwa waliweka ilani bandia ya kuajiri muuguzi na kisha kumhadaa mwanaume mmoja hadi barabara ya Karen kuelekea Miotoni ambapo walimwibia simu, pesa taslimu na bidhaa zingine.

DCI inasema wawili hao ni miongoni mwa genge la wahalifu ambao wamekuwa wakiwahadaa wakenya na msako wa washukiwa wengine umeanza.

Baadhi ya wakenya wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kulalama kuwa washukiwa wamekuwa wakiwaibia pesa zao baada ya kuwahadaa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here