Washukiwa wawili wanaohusishwa na mauji ya Kelvin Omwenga katika eneo la Kilimani, Nairobi watazuiliwa kwa siku 12 zaidi.
Hakimu mkuu mkaazi wa mahakama ya Kibera Derrick Kuto ameridhia ombi la upande wa mashtaka kuruhusu wawili hao Robert Bodo na Chris Obure kuzuiliwa zaidi ili kuruhusu kufanyika kwa uchunguzi.
Ouko aliifahamisha mahakama kwamba risasi iliyomuua Omwenga ilifyatuka kimakosa wakati walikuwa wanapigania bastola.
Polisi aidha wanachunguza sakata ya dhahabu ambayo inahusishwa na tukio hilo.