Washukiwa wa mauaji ya Willie Kimani wataka dhamana tena

0

Washukiwa wa mauji ya wakili Willie Kimani mteja wake pamoja na dereva wa teksi wanaitaka mahakama kuwaachilia kwa dhamana kesi yao ikiendelea.

Watuhumiwa hao wanaojumuisha maafisa wa Polisi wamekuwa wakizuiliwa tangu mwaka 2016.

Wanahoji kuwa wako katika hatari ya kupata tena ugonjwa wa corona kwa sababu ya kuendelea kuhudhuria vikao vya kesi hiyo.

Hata hivyo upande wa mashtaka umepinga ombi hilo ukisema kesi hiyo umefikia katika hatua muhimu kwani tayari mashahidi 44 wameitwa na imebakia mmoja tu.

Wanne hao ni maafisa wa Polisi Fredrick Leliman, Sylvia Wanjiru, Leonard Mwangi na Stephen Cheburet.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here