Washukiwa wawili kwenye mauji wa Kevin Omwenga katika eneo la Kilimani, Chris Obure na Robert Bodo wameachiliwa kwa dhamana na mahakama ya Nairobi.
Obure ameachiliwa kwa dhamana ya Sh2M huku mlinzi wake wa kibinafsi Robert Bodo ameachiliwa kwa dhamana ya Sh500, 000 na wadhamini wawili wa kiasi sawa na hicho.
Jaji Jesse Lesiit amewapiga marufuku wawili hao dhidi ya kupatikana na silaha yoyote hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Aidha mahakama imewaagiza wawili hao wasidhubutu kuhitilafiana na uchunguzi kwenye kesi hiyo ikiwemo kuwasiliana na jamaa za marehemu.