Washukiwa 11 watoroka kutoka kituoni Bungoma

0

Maafisa wa polisi wanendesha msako wa kuwanasa washukiwa kumi na mmoja waliotoroka kutoka kituo cha polisi cha Bungoma siku ya Jumamosi.

Washukiwa hao walikuwa wanazuiliwa kwa makosa mbalimbali na tayari mmoja wao ametiwa mbaroni.

Mkuu wa polisi katika eneo hilo Wilson Nanga anasema maafisa waliokuwa wakilinda kituo hicho walipashwa habari na wafungwa wengine mwendo wa  saa tisa asubuhi kuwa wenzao walikuwa wanatoroka.

Washukiwa hao walichimba shimo kwa ukuta na kutumia kutoroka.

Polisi wanatoa wito kwa umma kuwasaidia kuwanasa washukiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here