Wanotumia vyeti bandia waonywa

0

Wakenya wametakiwa kukomesha tabia ya kununua vyeti bandia kwa minajili ya kutumia udanganyifu ili kupata kazi.

Onyo hili limetolewa na mwenyekiti wa mamlaka inayosimamia kufuzu Kilemi Mweria ambaye anasema mazoea hayo yamedunisha viwango vya masomo nchini kwani watu ambao hawajahitimu wanatumia njia za mkato kapata vyeti.

Mweria amesema vyeti vya wanachama wote wa halmashauri hiyo iliyoteuliwa na waziri wa elimu Profesa George Magoha vitakaguliwa upya kabla ya kuanza kukagua vyeti vya watumishi wengine wa umma.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here