Makachero kutoka idara ya upelezi nchini DCI wamewakamata washukiwa wawili waliombaka kwa zamu mwanamke mmoja hadi akafariki Jumamosi iliyopita kaunti ya Nakuru.
Katika taarifa, DCI wanasema wawili hao Bernard Korir mwenye umri wa miaka 32 na Nelson Langat mwenye umri wa miaka 40 wamekamatwa katika kijiji cha Chigamba, Ole Nguruone kufautia msako uliondeshwa na maafisa wake.
Inadaiwa kuwa wawili hao ni miongoi mwa genge la wanaume watano waliombaka kwa zamu mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 26 na kusababisha kifo chake.
Washukiwa wengine watatu wanatafutwa na maafisa hao.