Wanasiasa waonywa kwa kukiuka masharti ya kuzuia msambao wa Corona

0

Watu 48  wamepakutwa na virusi vya corona  kwa kipindi cha saa Ishirini na nne zilizopita baada ya sampuli 1,081 kupimwa.

 Katibu katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi anasema hii inafikisha 36,205 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kufikia sasa huku idadi ya waliopona ikifikia 23,198 baada ya kupona kwa watu wengine 176.

Idadi ya maafa imeongezeka na kufikia 624 baada ya kufariki kwa watu wawili zaidi katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Hayo yakijiri

Hakuna anayekulazimisha kuhudhuria mikutano ya kisiasa, muhimu ni kuzingatia kwamba ni jukumu la mtu binafsi kuzuia msambao wa virusi vya corona.

Ndio kauli yake katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu mikutano ya kisiasa inayoendelea kuandaliwa na wanasiasa licha ya kuwepo kwa mwongozo unaozuia mikusanyiko ya watu.

Dkt. Mwangangi vile vile amewarai viongozi kuwa katika mstari wa mbele kuzingatia masharti ya usalama ili kuzuia msambao wa virusi hivyo.

Nairobi ingali inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya visa vya ugonjwa huo wa corona ambapo kufikia leo, visa 19,990 vilikuwa vimeandikishwa, Kiambu ni ya pili kwa kuandikisha visa 2,634, Mombasa ni ya tatu kwa kuandikisha visa 2,603 ikifuatiwa na Kajiado iliyo na visa 1,934.

Elgeyo Marakwet na West Pokot ndizo kaunti ambazo zimeandikisha idadi ndogo ya visa vya ugonjwa huo kwa kuwa na visa saba kila mmoja.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here