Wanaotaka kujiunga na NYS sharti wapimwe corona na kupewa vyeti

0

Vijana wanaotaka kujiunga na kundi la vijana (NYS) Novemba mwaka huu wametakiwa kupimwa na kupewa vyeti sahihi vya Corona.

Kupitia kwa tangazo kwenye gazeti rasmi la serikali, mkurugenzi mkuu wa NYS Matilda Sakwa amesema mwongozo huo  umetolewa ili kupunguza usambazaji wa virusi vya Corona.

Sakwa amesema usajili utaanza tarehe 2 Novemba hadi tarehe 6 Novemba katika vituo 333 nchini huku usawa wa jinsia ukizingatiwa na mayatima kupewa kipau mbele iwapo watawasilisha vyeti vya vifo vya wazazi wao.

Makurutu watakao fuzu watasajiliwa kwa vyuo vya NYS Gilgil na Naivasha kuendelea na mafunzo yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here