Wanaharakati wa Kupinga Mhadarati wa Tumbaku wanataka serikali kufanyia marekebisho Sheria ya Kitaifa ya Kudhibiti Tumbaku na Nikotini ya Mwaka wa 2007 ambayo wanadai imepitwa na wakati.
Marekebisho haya wanasema itapiga jeki juhudi za kulinda afya ya umma.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa Bodi ya Kudhibiti Tumbaku(T.C.B) Naomi Shabaan Wanaharakati hao wamesema sheria iliyopo ya udhibiti wa Tumbaku haitoi ulinzi wa kutosha kukabiliana na bidhaa zinazoibuka za Nikotini zinazosambaa humu nchini.
“Tunatoa wito kwa serikali kuzingatia, kodi hizi kama chanzo cha mapato kwa ajili ya kuongeza nakisi ya mapato kwa sababu bado tunayo nafasi ndefu ambayo sigara na bidhaa za tumbaku zinaweza kutozwa kodi,” amesema Naomi.
Baadhi ya bidhaa zinazoibuka za nikotini ambazo sheria hio haitoi mwongozo kuhusu jinsi ya kudhibiti ni Pamoja na sigara za kielekroniki, pochi za nikotini na shisha.
“Tuligundua Sheria ya kudhibiti tumbaku, iliyopitishwa mwaka 2007, imepitwa na matukio, bidhaa hizo mpya ni za kiubunifu na hazikufikiriwa mwaka 2007 na hivyo ni lazima tufanye marekebisho ya Sheria ya kudhibiti tumbaku ili tuweze kuendana na bidhaa mpya sokoni,” amesema Andrew Toro, mkuu wa idara ya madawa za kulevya.
Wawili hao wamezungumza wakati wa kongamano la 3 la ushuru wa tumbaku katika kaunti ya Nairobi.
STORY BY : JACINTA MUSYOKI