Polisi wanawazulia wanaharakati kadhaa waliokamatwa mapema hii leo wakati wa maandamano ya kupinga kuibiwa kwa pesa za kukabiliana na janga la COVID19.
Maafisa wa usalama walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wanashinikiza kukamatwa na kushtakiwa kwa watu wote wanaodaiwa kuhusika na wizi wa pesa hizo.
Waandamanaji hao walikuwa wanapanga kuandamana kuanzia katika eneo la Freedom Corner kwenye bustani ya Uhuru na kufululiza hadi katika Afya House kuliko na afisi za wizara ya afya.