Wanahabari walidhulumiwa Kenya wakati wa corona

0

Wanahabari 48 wa kampuni mbalimbali za habari walivamiwa wakiwa kazini wakati taifa likipambana na janga la COVID19.

Haya ni kwa mujibu wa ripoti iliyozinduliwa na shirika la Article 19 ambalo linasema miongoni mwa wanahabari waliovamiwa ni wanaume 34 na wanawake 14.

Mkurugenzi wa shirika hilo la Article 19 ukanda huu wa Afrika Mashariki Mugambi Kiai anasema wengi wa wanahabari walikamatwa, kupata vitisho kupitia njia ya simu, kupigwa, kunyimwa uhuru wa kupata taarifa za umma miongoni mwa dhuluma zingine.

Wanahabari 22 kati ya 48 walidhulumia mwezi machi hadi mwishoni mwa mwezi wa Aprili, wiki sita tu baada ya mlipuko wa virusi vya corona nchini.

Kaunti ya Nairobi imeathirika zaidi na uvamizi wa wanahabri ikirekodi visa 16 vya waandishi hao kudhulumiwa, Mombasa 7, Turkana 5, Uasin Gishu, Nakuru , Embu na Kisumu 3.

Kiai anaituhumu serikali kwa kufeli kutekeleza jukumu lake la kuwalinda wanahabari na kuongeza kuwa wanafaa kupata habari kwa njia huru na sahihi haswa kuhusiana na jinsi serikali imekuwa ikikabiliana na janga la corona.

Aidha, Utafiti huo umeonyesha kuwa kuanzia Octoba 2019 hadi Machi 2020 Dhuluma za wanahabari zimeongezeka zaidi ikilinganishwa na miaka iliyopita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here