“Wanafunzi wako salama zaidi shuleni kuliko nyumbani” – Sossion

0

Katibu mkuu wa chama cha walimu nchini KNUT Wilson Sossion amewataka washikadau wa elimu kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanarejea shuleni wakati shule zitafunguliwa hivi karibuni.

Sossion ametoa changamoto kwa walimu wanaorejea shuleni siku ya Jumatatu kufahamu waliko wanafunzi wote ikiwemo wa kike ambao walipata ujauzito ili warejee shuleni kukamilisha masomo yao.

Sossion amesema kuwa wanafunzi watakuwa salama shuleni kuliko walivyo nyumbani kwani anadai kuwa baadhi ya wazazi wameshindwa na jukumu lao la ulezi.

Sossion pia ameitaka wizara ya elimu kuwa na kitengo cha kushughulikia masual ya kijisnia katika tume ya huduma za walimu TSC na kuahidi kuwa muungano wa KNUT utakuwa na afisa wa jinsia katika kila shule kuwasaidia wanafunzi ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo dhulma za kimapenzi.

Visa kadhaa vya wasichana kupachikwa mimba viliripotiwa katika maneo mbalimbali nchini baaa ya shule kufungwa kufuatia janga la corona.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here