Wanafunzi 52 wa shule ya Kolanya, Busia wakutwa na corona

0

Wanafunzi 52 wa shule ya wavulana ya Salvation Army Kolanya kaunti ya Busia wamekutwa na virusi vya corona.

Wengine waliopatikana na virusi hivyo baada ya kupima sampuli 100 ni walimu sita na wafanyikazi wawili.

Gavana wa kaunti ya Busia Sospeter Ojamoong anasema waliopatikana na ugonjwa huo wamejitenga ndani ya shule hiyo huku wahudumu wa afya wakitumwa kuwashughulikia.

Ojamoong anasema kufikia sasa kaunti ya Busia imeripoti visa 1,683 vya ugonjwa huo baada ya kupima sampuli 75,564.

Waziri wa elimu Profesa George Magoha amepuuzilia mbali uwezekano wa kufunga shule licha ya visa vya ugonjwa wa corona kuripotiwa shuleni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here