Takriban wanafunzi alfu tatu hawajaripoti shuleni katika kaunti ya Baringo siku moja baada ya shule kufunguliwa.
Akizungumza alipozuru kaunti hiyo kutathmini hali kufuatia mafuriko Jumanne, katibu mkuu katika wizara ya elimu Belio Kipsang’ amesema wanafunzi walioathirika watahamishwa hadi katika shule zingine kuendelea na masomo yao.
Kipsang’ amesisitiza kwamba hakuna mwanafunzi anafaa kufukuzwa shuleni kwa sababu ya kukosa karo.
Mkutano mwingine na maafisa wa elimu utaandaliwa Alhamisi wiki hii kutafuta suluhu kwa swala hilo.