WAMPANGIA RUTO; VIONGOZI WA UPINZANI WAKUTANA KUJADILI MIKAKATI YA 2027

0

Viongozi wa upinzani wamekutana leo hii kupanga mikakati ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua, kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, kiongozi wa chama cha DAP-K Eugene Wamalwa, Seneta wa kaunti ya Kisii Richard Onyonka na kiongozi wa chama cha Safina Jimmy Wanjigi.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X, Gachagua amesema kuwa wanauelewa wa mahali ambapo taifa linapaswa kuwa na wako tayari kuongoza nchi kuelekea njia hiyo.

“Asubuhi ya leo Kiongozi wa Chama cha Ukombozi PLP Martha Karua amechukua jukumu lake kama Mratibu wetu alipotuleta pamoja kuendeleza kazi ya kuikomboa nchi hii kutoka kwa minyororo ya utawala mbaya na ufisadi.” Amesema Gachagua.

Gachagua mara si moja amekariri kuwa lengo lake na viongozi watakaojiunga naye kwenye muungano wa kisiasa ni kumtuma Rais William Ruto nyumbani.

“Kama timu tunaelewa Wakenya wanataka tuende wapi na kwa nini, na tunachohitaji kufanya ili kufika huko. Pia tuko wazi kabisa juu ya nini lengo letu la msingi ni, katika safari ya kufika tunakokwenda kama nchi.

Viongozi hao wanakutana wakati ambapo kinara wa chama cha ODM Raila Odinga anatarajiwa kutangaza mwelekeo wake wa kisiasa wakati wowote kuanzia sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here