Wambugu ataka Ruto achunguzwe

0

Mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu anaitaka idara ya upelezi DCI kuwachunguza wanasiasa wanaotumia lugha ambayo huenda ikasababisha ghasia kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.

Katika barua kwa mkurugenzi mkuu wa DCI George Kinoti, mbunge huyo ameelezea wasiwasi wake kuwahusu wanasiasa wanaotumia matamshi kama ‘watu fulani’ na ‘watu wengine’.

Mbunge huo husan kwenye barua yake amewataja naibu rais William Ruto, mbunge wa Kapseret Oscar na mwenzake wa Emurua Dikkir Johana Ng’eno kwa kuwa na mazoea ya kutumia matashi hayo.

Ngunjiri katika barua yake anasema matamshi hayo yanafanana na ‘madoadoa’ na ‘kwekwe’ ambaye yalisababisha ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2017.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here