Waluke kufahamu hatma yake Jumatatu

0

Mbunge wa Sirisia John Koyi Waluke pamoja na mshtakiwa mwenza Grace Wakhungu watasubiri hadi Jumatatu wiki ijayo kufahamu hatma yao.

Hii ni baada ya jaji John Onyiengo kuhairisha kutoa uamuzi kuhusu ombi lao la dhamana uliokuwa utolewe Ijumaa kufuatia zoezi la kupulizia dawa mahakama ya Milimani lililofanyika.

Waluke alihukumiwa miaka 67 jela au alipe faini ya Sh1b huku Wakhungu akihukumiwa miaka 69 jela au alipe faini sawa na hiyo baada ya kupatikana na hatia kwenye sakata ya mahindi katika shirika la nafaka na mazao NCBP ambapo Sh313M zilifujwa.

Wawili hao walikata rufaa dhidi ya uamuzi huo huku Waluke akiiambia mahakama kwamba yeye ni mbunge na kwamba kwa kuzingatia umri wake sawa na afya yake mahakama hiyo inafaa imuwachilie kwa dhamana.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here