Washukiwa wanne wa genge ambalo limekuwa likiwaibia watu kwa kuwahadaa kupitia kwa mapenzi ya mtandao wanatazamiwa kufikishwa mahakamani hii leo.
Wanne hao Bernard Mbunga, Fredrick Mutiso, Catherine Mumbi na Kelvin Nzioki walikamatwa mtaani Ruaka hapo jana na maafisa kutoka idara ya upelelezi nchini DCI wakimwibia raia wa Uturuki.
DCI inasema raia huyo wa kigeni alihadaiwa na Mumbi kwamba wangekuwa na uhusiano wa kimapenzi na badala yake wakampeleka hadi nyumba moja na kuanza kumtesa kabla ya kumwibia pesa alizokuwa nazo na pia kwa simu huku mshukiwa wa nne akinaswa kwa mtambo wa ATM tayari kutoa pesa kwa akaunti ya mshukiwa.
Washukiwa hao wanatazamiwa kufunguliwa mashtaka ya ulaghai na pia wizi.