Asasi za uchunguzi zimetakiwa kuharakisha uchunguzi na kuwaadhibu waliohusika na wizi wa pesa zilizolenga kupambana na janga la COVID19.
Allan Maleche ambaye ni mkurugenzi wa mkuu wa shirika linaloshughulikia waathiriwa wa virusi vya HIV (KELIN) mojawapo ya mashirika ambayo yamekuwa yakishinikiza uwajibikaji kuhusu matumizi ya pesa hizo amesema wahusika wanafaa kushtakiwa na pia kurejesha pesa walizoiba.
Maleche aidha anamtaka mkaguzi mkuu wa hesabu za umma Nancy Gathongo kufanya ukaguzi katika wizara ya afya kufuatia madai ya kuporwa kwa pesa za kupambana na virusi vya UKIMWI na TB.