Walemavu wataka maoni yao yajumuishwe kwenye BBI

0

Watu wanaoishi na ulemavu wanataka ripoti ya BBI kufanyiwa marekebisho ili kuyapa kipau mbele maswala yanayowahusu.

Seneta maalum Isaac Mwaura anayewaakilisha bungeni watu wenye ulemavu anasema wanauanga mkono ripoti hiyo ila ni sharti ifanyiwe marekebisho na kujumuisha maslahi yao ikiwemo nafasi yao kwenye nyadhifa za uongozi.

Mwaura vile vile amewataka vijana kuendelea kusukuma kujumuishwa kwa maslahi yao kwenye ripoti hiyo inayopendekeza kubuniwa kwa tume ya vijana kushughulikia maswala yao.

Na huku visa mbalimbali vya wanafunzi kuambukizwa virusi vya corona vikiendelea kuongezeka, Mwaura anaitaka serikali kufunga shule hadi mwaka ujao ili kuwalinda wanafunzi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here