Wakuu wa usalama wahamishwa

0

Wakuu mbali mbali wa usalama wamehamishwa kwenye mabadiliko yaliyotangazwa na waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiangi kufuatia mashauriano na rais Uhuru Kenyatta.

Kwenye mabadiliko hayo, Moffat Kangi na aliyekuwa mkuu wa usalama Nairobi Wilson Njega wameteuliwa kuwa makatibu katika wizara ya usalama.

Naye aliyekuwa kamanda mkuu eneo la Nyanza James Kianda amehamishwa hadi Nairobi kwa wadhifa uo huo.

Magu Mutindika na Esther Maina wamehamishwa hadi Nyanza na Magharibi mtawalio kuwa makamanda wakuu wa Polisi.

Makamishna wa kaunti waliohamishwa ni kama ifwatavyo;

 1. Onesmus Kyatha amehamishwa kutoka kaunti ya Mandera hadi Mombasa
 2. Joshua Nkanatha amehamishwa kutoka Kajiado hadi Marsabit
 3. Michael Tialal amehamishwa kutoka kaunti ya Siaya hadi Garissa
 4. Gilbert Kitiyo amehamishwa kutoka Mombasa hadi Mandera
 5. Stephen Kihara amehamishwa kutoka Kisii hadi Uasin Gishu
 6. Mwangi Meru amehamishwa kutoka Garissa hadi kaunti ya Narok
 7. George Omoding amehamishwa kutoka kaunti ya Bomet hadi Kakamega
 8. Samuel Kimiti amehamishwa kutoka Narok hadi kaunti ya Bungoma
 9. Olaka Kutswa amehamishwa kutoka Nandi hadi kaunti ya Kilifi
 10. Boaz Cherutich amehamishwa kutoka Nyandarua hadi kaunti Migori
 11. Abdirizak Jaldesa amehamishwa kutoka Uasin Gishu hadi kaunti ya Kisii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here