Wakenya wapoteza ajira kutokana na corona

0

Wakenya million moja nukta saba walipoteza ajira kati ya mwezi Aprili na June mwaka huu 2020.

Haya ni kwa mujibu wa shirika la kitaifa la takwimu KNBS ambalo linasema kuwa viwango vya ukosefu wa ajira vimepanda hadi asilimia 10.4% kutoka asilimia 5.2% mwezi Machi mwaka huu.

Shirika hilo sasa linasema kuwa wakenya ambao wameajiriwa ni million 15.9 ikilinganishwa na wakenya 17.8 waliokuwa na ajira kufikia mwezi Machi.

Shirika hilo limeongeza kuwa wakenya ambao hawajakuwa na ajira kwa zaidi ya mwaka mmoja imeongezeka na kufikia watu 551, 563.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here